JB Masanduku kufunga ndoa siku yenye mamake aliaga dunia

Tina-Kaggia-JB-Masanduku
Tina-Kaggia-JB-Masanduku

Mipango ya Harusi yake JB Masanduku inayotarajiwa kufanyika tarehe 11 mwezi Novemba imekamilika na mambo yote yako seti.

Hata hivyo, harusi hio ilifaa kufanyika tarehe 24 mwezi wa nane siku ya kuzaliwa ya mpenziwe Jackie Karanja lakini sasa itafanyika tarehe 11 mwezi Novemba siku aliyoaga dunia mamaye mzazi.

"Hii ni siku spesheli ya mamangu mzazi na ningependa sana kumpa heshima zake huku pia nikitaka kumfurahisha mpenzi wangu,"Alisema JB  masanduku. JB pia anasema kuwa  mpenziwe angetamani sana kumuona mamaye mzazi aliyeiaga dunia.

"Nimezungumza na watu wangu na wakanihakikisHia kuwa mambo yote yapo tisti. Mke wangu aliamua kumpa heshima mamangu kwa kuichagua siku aliyoniacha mama."

 JB anamesema kuwa mamake mzazi alimsaidia kuwa na uulivu kila wakati kwani alijua kuwa haraka haraka haina baraka. Kwenye harusi yake, JB amewaalika watu mashuhuri huku naibu rais akiwa wakwanza kukubali wito wake.

"Nilipomwalika naibu rais alikubali kwa haraka."
Wengine wanaotarajiwa kuhudhuria harusi hio ni pamoja na Churchill, Betty Kyalo, Dj Shiti pamoja na Teacher Wanjiku. Harusi hio itakuwa na mavazi spesheli ya rangi ya udhurungi huku pia wavunja mbavu waliofanya kazi na babaye mzazi wakitarajiwa kuhudhuria.
JB alipatana na mkewe mwaka uliopita na mwanzoni mwa mwaka huu JB alilipa mahari yake Jackie ambaye ni mwigizaji wa stesheni moja humu nchini.