Je, Ruto kawaudhi GEMA? Sababu zao kumtaka ajiuzulu wadhifa wa naibu rais

ruto
ruto
Tegemeo la William Ruto kupata uungwaji mkono na jamii ya GEMA huenda likagonga mwamba mwaka wa 2022. Hii nikufuatia tetesi kutoka kwa wabunge wa kundi hili kusema kuwa kiongozi huyu anafaa kujiuzulu haraka iwekanavyo. Kundi hili kupitia kwa mwenyekiti wao Lawi Imathiu linashikilia msimamo kuwa siasa za mapema za TangaTanga zinaathiri kwa kiasi kikubwa lengo lake rais Kenyatta la kufanya maendeleo nchini.

Soma hapa :

Imathiu sasa anahoji kuwa kundi la TangaTanga na wandani wa naibu rais wanalenga kuwagawanya wananchi wa Gikuyu, Embu na Meru.

 “Ni lazima tuwe makini sana kwa nguvu zilizo na nia mbovu ya kugawanya jamii yetu." Alisema kiongozi huyo huku akiwahimiza viongozi wa mlima Kenya kugoma siasa na kufuata amri ya rais Kenyatta ya kutofanya kampeni za mapema.

Imathiu alisisitiza kuwa Uhuru Kenyatta ndiye kiongozi wa GEMA kwa sasa na wakati ujao. Katika maazimio ya kupata kiti cha urais 20222, Ruto anapania kurithi kura za mkoa wa kati kutoka kwa bosi wake kwa mujibu wa mkataba uliofanyika kabla ya kuunda chama cha Jubilee.

Ila kwa jicho la mbali huenda lengo hili likabuma ukizingatia misimamo ya "Hatuna Deni ya mtu" kutoka kwa viongozi kutoka eneo hilo.

“Mwelekeo wa jinsi mambo yanavyokwenda kisiasa hayalingani na lengo la Rais wetu Kenyatta na taifa kwa jumla." Imathiu alisema.

Soma hapa pia:

Kiongozi huyu aliwaambia TangaTanga , kundi ambalo linahusishwa na naibu wa rais kuheshimu msimamo wa" baada ya uchaguzi, viongozi wote wagome siasa na kuliendesha taifa."

“Tunaomba watu wa GEMA hususan wanasiasa wagome kushiriki siasa za mapema na wamakinike katika juhudi za maendeleo kwa wananchi." Imathiu.

“Hii ni hali mbaya zaidi inayosababishwa na Ruto mwenyewe. Ameitoa kadi hatari sana na DCI wanatakiwa wamtie nguvuni." alisema mbunge wa Tiaty ,William Kamket.