Je, una mazoea ya kununua matunda na kuyala barabarani? Tazama hii video

FotoJet (2)-compressed
FotoJet (2)-compressed
Watu wengi sana hununua matunda yanayouzwa na wachuuzi barabarani na kuyala hususan wanapokuwa safarini.

Ijapokuwa matunda ni mojawapo ya viungo muhimu ya lishe bora, yanaweza yakasababisha maradhi hatari mwili.

Katika kanda ya video hii, mchuuzi anaonekana akiyaosha matunda kwenye maji chafu ya mtaro kando ya barabara.

Aidha, baada ya kuyaosha, lengo lake ni kwenda kuyauzia wapita njia au hata abiria walio na kiu ya kuyala matunda.

Hivyo basi, unafaa kuwa mwangalifu sana, usije ukajipatia maradhi hatari zaidi kutokana na maji taka yatumiwayo kuosha matunda hayo.