Je wajua waweza ishi kwa mda mrefu kwa kuwa mkarimu?

ukarimu
ukarimu

Ukarimu gani unaweza kuufanya? Je, ni sawa mtu kuonyesha hisia zao?

Inawezekana kuna ukweli , wanasayansi na wasomi katika kituo cha utafiti wanasema kuwa mtu anaweza kufanya mambo mengi zaidi ya ukarimu na kuongeza muda wa kuishi .

Wafanyakazi wa taasisi ya ukarimu ya Bedari iliyopo chuuo kikuu cha California, huko Los Angeles (UCLA) wako tayari kwa ajili ya utani.

"Tukiangalia upande wa kisayansi . Ni kama tuko kwenye mzunguko, hapa tunazungumzia upande wa kisaikolojia na kibaiolojia," Daniel Fessler,mkurugenzi wa taasisi anaeleza.

Suala la mtu kuwa mkarimu limeweza kuchukua vichwa vya habari hivi karibuni.

Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama anasema kuwa:

"Kuwa jasiri ni ukarimu. Hakuna ubaya kwa mtu kuwa dhaifu au kuwa na huruma," alisema.

"Mtu kuwajali watu wengine si udhaifu. Ni jambo jema , tunapaswa kujali wengine kwa kuwa na uadilifu na kuwajali wengine kwa heshima."

Ellen DeGeneres aliwahi kuzungumzia ukarimu wakati akizungumzia urafiki wake na George W Bush: "Ninaposema kuwa mkarimu, 'Unapaswa kuwa mkarimu kwa wengine, simaanishi kama watu wanafikiria sawa na vile wanavyotenda. Ninachomaanisha ni kwamba uwe mkarimu kwa kila mtu bila kujali.'"

Leo ikiwa siku ya ukarimu duniani (Novemba 13) Tunaangazia ukarimu una maana gani - na kujiuliza kwa nini ni muhimu?

Hilo ndilo jambo ambalo wataalamu wanataka kufanyia utafiti.

Je wako makini , je ni suala ambalo linaingatia uhai na vifo vya watu.

Kazi ya bwana Fessler ilikuwa ni kuangalia namna ambavyo watu wanaweza kushawishika kufanya vitendo vya ukarimu, kwa kushuhudia fadhila na kueneza ukarimu.

"Nadhani ni sawa kusema kuwa tunaishi katika umri ambao sio rafiki," alisema.

"Duniani kote , kile tunachokiona ni ongezeko la migogoro baina ya watu ambao wana maoni tofauti katika masuala ya kisiasa au tofauti za kiimani."

Ukarimu, anasema kuwa ni "fikra, hisia na imani ambayo ina uhusiano na hatua ambazo zinaweza kuwanufaisha wengine, Kuwanufaifa wengine haimaanishi kuwa ndio mwisho."

Soma mengi