Jibaba La Miaka 30 Lashtakiwa Kwa Kumlazimisha Mtoto Ampapase Sehemu Nyeti

Mwanamume wa umri wa miaka  30 ameshtakiwa kwa kutekeleza tendo lisilo la kawaida na mtoto. James Wasike anadaiwa kumlazimisha mtoto wa miaka 12 kumbusu na kumgusa sehemu zake za siri akiwa nyumbani kwake Julai  22.

Pia anadaiwa kumvua nguo mtoto huyo na kumpapasa sehemu zake nyeti.

Mtoto huyo alikuwa ametumwa na mamake kuchukua pesa kutoka kwa rafikiye na ndipo Bwana Wasike alipomlazimisha kwenda nyumbani kwake.

Wasike alijaribu kumziba mdomo asipige kelele  wakati alipokuwa akimvua nguo na hapo majirani wakavunja mlango na kumwezesha mtoto hyo kutoroka na Wasie akakamatwa. Hata hivyo amekana mashtaka na kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki tatu.