Jicho la EACC! Maafisa wa EACC wawatia mbaroni wafanyakazi wa kaunti ya Kilifi

EX4wN6EWAAE0C8A (1)
EX4wN6EWAAE0C8A (1)
Ni siku chache tu zilizopita ambapo shughuli ya kuwapima wakaazi wa kaunti ya Kilifi kuhusiana na virusi vya Corona ilisitishwa kwa kukosekana na vifaa vya kufanikisha shughuli hiyo. Hii leo maafisa kutoka tume ya maadili na kupambana na ufisadi EACC imewatia mbaroni maafisa wakuu wa kaunti ya Kilifi kwa kukosa kuwasilisha stakabadhi za matumizi ya pesa ya kununua vifaa vya kuwapima wakaazi.

Kilifi ni miongoni mwa kaunti ambazo serikali ilituma pesa za kusaidia kukabiliana na janga la corona baada ya kuandikisha idadi kubwa ya maambukizi japo kwa sasa ilipungua.

Hatua ya kulemazwa upimaji wa watu kwenye kaunti hiyo kuliibua hisia mseto haswa baada ya kubainika wazi kuwa serikali ilikuwa imetoa ufadhili.

Hata hivyo, wizara ya afya imejikuta chini ya shinikizo baada ya kudaiwa kuwa pesa zilizotumwa na mashirika mbalimbali kwa kusaidia vita dhidi ya corona ziliibiwa na zingine kutumika vibaya.