Jinisi ya kuziosha na kuzitunza rasta zako.

Rasta ni mtindo maarufu kwa watu wengi siku hizi.  Wengi huweka rasta kwa sababu mbali mbali kama vile sababu za kidini huku wengine wakiweka zile ambazo sizakudumu akiaminika zinasaidia kukuza nywele. Mara tu unapoamua kuweka rasta, ni muhimu kuzitunza ili kuhakikisha kuwa zinaendelea kukua na tena zenye afya. Kama nywele nyingine yoyote, unapaswa kuzisafisha rasta zako mara kwa mara kwa kutumia bidhaa na mafuta yanayofaa ili kuwa na nywele yenye afya. Hizi hapa njia sita za kuhakikisha unatunza rasta zako.

Zioshe rasta zako baada ya kila siku mbili hadi nne. Hakikisha kwamba unaziosha rasta zako angalau siku moja kwa wiki lakini sio kila siku. Kisha subiri angalau siku mbili baada ya kila mwosho mmoja ili kuruhusu ngozi ya kichwa chako kuwa na mafuta. Iwapo una nywele iliyokauka ambayo mara nyingi huenda ikasababisha nywele zako kukatika, zungumza na msusi wako kuhusu ni mara ngapi unapswa kuwa ukiziosha nywele zako kulingana na aina ya nywele yako.

Zimwagilie nywele zako maji yaliyo na joto.  Katika bafu zinyunyizie nywele zako maji yaiyo na joto maji hayo hayapaswi kuwa mto sana na usiziweke nywelel zako kwa maji kwa muda mrefu zana kwa wakati mmoja. Kuziweka nywele zako kwa maji kabisa kunaweza kusababisha nywele kuwa nzito sana na kufanya kuwa vigumu kuzikausha .

Mwaga tone robo ya sabuni ya kuosha nywele yaani shampoo katika kichwa chako. Anza na kiasi kidogo cha shampoo, na uigusishe kidogo tu kwa nywele zako. Poleza shampoo kwenye rasta zako, lakini usizisugue rasta unapoziosha. Iwapo unahishi ni kama huna shampoo ya kutosha unaweza kuongeza. Shampoo isiyo na mabaki husaidia kusafisha uchafu na kusaidia rasta zako kuwa bila hofu ya kuacha nyuma safu ya sabuni hiyo.

-Wachacha shampoo ikae kwenye nywele zako kwa dakika 1-2. Kabla ya kusuuza nywele zako, wacha shampoo ikae kwenye nywele zako kwa dakika moja au mbili. Hii itahakikisha kuwa inaondoa uchafu wote na mafuta kwa nywele. Iwapo una nywele chache ama ngumu, kaa na sabuni hiyo kwa angalau dakika moja kuzuia sabuni hiyo kusafisha nywele zaidi kwa sababu huenda zikafumuka.

 - Suza rasta zako vizuri baada ya kutumia sabuni. Zisuze rasta zako baada ya kuzimwagilia sabuni. Unapozisuza, zifinye ili kuhakikisha sabuni yote imetoka. Endelea kuaosha hadi sabuni yote iishe nyweleni.

Kausha maji kutoka kwa nywelel kwa kuzifinya. Baada ya kuhakikisha kuwa rasta zako ni safi, zifinye ili kuondoa maji kisha tumia taulo au kitambaa chochote kuzikausha zaidi. Usizishikilie au kuzifunga na rasta  kama bado hazijakauka, la sivyo zitanuka. Iwapo una wasiwasi kuwa huenda nywele zako zikanuka hata bila ya wewe kuzifunga unaweza kuzinyunyizia mafuta.