Jinsi ya kuunda viatu aina ya Akala, ubora wake

Ni viatu ambavyo vimetumika na jamii mbali mbali ikiwemo Maasai, Samburu, Pokot na kadhalika.

Viatu vya akala si nzito unapovivaa, na vinaweza tumika mahali popote kulingana na mtu yeyote yule anavyopenda.

Je, viatu hivi hutengenenzwa vipi?

Soma habari zaidi:

Na vifaa gani hutumiwa?

Akala hutengenezwa kutoka kwa mabaki ya magurudumu ya gari yaliyochakaa hivo basi hayawezi kutumika barabarani tena.

Magurudumu hayo huchongwa mchongo wa viatu kisha baadaye yanalainishwa vizuri.

Kila jozi ya viatu huwa imeundwa kutumia mkono kwa uangalifu mkubwa.

Ngozi kutoka bidhaa zingine pia hutumiwa wakati viatu hivi vya Akala vinaundwa, ili kuipa viatu hivo urembo ama umaridadi ambao utavutia wateja kuvinunua.

Kazi ya kutengeneza Akala pia ina changamoto yake, kwani vifaa kama visu ambavyo wasanii hao hutumia kuchonga viatu ni hatari sana.

Hivo basi yeyote yule anayejishughulisha na kazi kama hiyo anapaswa kuwa makini.

Viatu hivi pia vimeonekana kuwa kivutio kikubwa kwa watalii kutoka nchi mbali mbali, jambo ambalo limesaidia kuinua hali ya maisha ya wachuuzi wa viatu hivi kwa kuziuza.

 Mhariri:Davis Ojiambo