John Kibera asimulia jinsi maiti ilimshika alipojaribu kuiba jeneza

john kibera
john kibera
Aliyekuwa mwizi sugu wa majeneza, John Kibera aliwashangaza sana waskilizaji wa Radio Jambo aliposimulia maisha yake ya ujambazi, kabla ya kubadilisha njia zake.

Akizungumza na mtangazaji Massawe Japanni katika kitengo cha Ilikuwaje, Kibera ambaye sasa ni mhubiri, alisimulia kuwa aliwahi fungwa jela la watoto akiwa na miaka kumi na mitatu kwa kumuibia shangaziwe shilingi mia moja hamsini na humo ndio alipopata wazo la kuwaibia wafu jeneza.

Kibera alieleza kuwa kati ya wenye aliowafunza wizi, yeye pekee ndiye aliye uhai kwani wengine wote waliaga dunia baada ya kujihusisha na shughuli ya wizi.

Cha kushangaza ni kuwa Kibera ambaye ni mzaliwa wa Kawangware aliwahi jipata taabani akiwa katika shughulo ya kuiba jeneza katika maeneo ya Kendu Bay kaunti ya Homa Bay.

Alieleza jinsi aliwahi vamiwa na maiti ndani ya kaburi na alilazimishwa kutimua mbio huku akiiwachia shati yake kwa hofu na mshtuko mkuu.

Alisimulia:

Maiti ya Jaluo na Kisii hapana,  hata ya waluhya hapana.

Ni ukweli, nilienda mimi mwenyewe kule Kendu Bay kwenda kujaribu kutoa jeneza usiku maiti ikaniletea shida nikaikimbia nikaiwachia shati. Niliona maiti imefura inataka kunishika nikaiwachia shati. Ni ukweli maiti za jaluo husumbua.

Hata ilibidi mara ya mwisho nifanyiwe tambiko maalum. Ambapo nilitoa ng'ombe sita na mbuzi na kuku kadhaa nikaambiwa nipige magoti kwa ile kaburi nimwambie yule mfu pole.

Si unajua yule mjaluo nilikuwa nimemsumbua nikienda kulala anakuja kunisumbua, ni ukweli wako hivyo.

Nilifanyiwa tambiko kubwa sana ili waweze kubeba ile roho. Nilienda kwa ile familia nikatafuta wazee nikawaambia huyu mfu wenyu ananisumbua. Wakaniambia basi kama ulikuwa umekuja kumuibia huyu mfu lazima tufanye tambiko maalum ya kwenda ukamwambie pole.

Skiza mahojiano yote katika kanda ifuatayo.

&feature=youtu.be