Joyce Omondi na Waihiga wafichua mbona uhusiano wao ulikuwa siri kuu

waihiga (2)
waihiga (2)

Mashabiki kila mara wamekuwa wakikimbilia kupata ujumbe wowote wa wapenzi wawili wa runing, Waihiga Mwaura na mkewe Joyce Omondi.

Na hii ni kwa sababu wawili hao wamekuwa wakiweka maisha yao ya ndoa kuwa siri kuu.

Ni mambo kidogo sana yanayojulikana kuhusu mapenzi au uhusiano wao, na hiyo ndio sababu licha ya kuwa katika mwanga wa wakenya, waliweza kuweka uhusiano wao chini ya maji hadi siku chache kabla ya harusi yao.

Wapendwa hawa wawili walianza kuchumbiana wakiwa katika runinga ya Citizen, Waihiga akiwa mwandishi wa michezo huku Joyce akiwa mtangazaji wa kipindi cha injili cha Rauka.

Katika mahojiano ya hivi karibuni na jarida la Salon, wawili hao walifichua sababu yao ya kuweka uhusiano wao kama siri kuu.

Tuliamua kujiwekea na hatungewahi chapisha picha au ujumbe wa mwenzetu ila tu kama ingekuwa siku za kufana. Chochote kizuri lazima kifichwe na hiyo ndio imekuwa sera yetu. Wawili hao walisema.

Waihiga na Omondi pia walifichua kuwa wafanyikazi wenzao pia hawakujua kuwa wanachumbiana hadi walipofunga pingu za maisha.

Tuliamua kujiwekea maneno ya uhusiano wetu kutoka mwanzo. Watu wengi (Pamoja na wafanyikazi wenzetu) hawakujua kuwa tunachumbiana hadi tulipofunga ndoa. Walisema huku wakiongeza hiyo ndio kwa sababu haya ni mahojiano ya kwanza na ya mwisho tutafanya pamoja kwa mda mrefu.

Wawili hao waliliambia jarida hilo kuwa walikutana mwaka wa 2012 siku ya jumapili asubuhi wakti Joyce alikuwa anaondoka baada ya kuandaa shoo yake.

Waihiga alimnyemelea mwimbaji huyo wa nyimbo za injili kwa mda lakini bado alikuwa anadinda kuingia katika uhusiano naye.

Hatimaye alikubali na wakaanza kuchumbiana kisiri kabla ya kuoana Disemba 18, 2015 katika hoteli ya Sawela, Naivasha.