Kaunti ya Kakamega ya anza uchunguzi kubaini swala la wasichana 'mapacha'

Kakamega County
Kakamega County
Serikali ya kaunti ya Kakamega imeanzisha uchunguzi kubaini ukweli unaozingira uzo wa wasichana wawili wanaosemekana kuwa mapacha waliozaliwa katika hospitali kuu ya Kakamega miaka ishirini iliyopita

Waziri wa afya katika serikali ya kaunti ya kakamega recho okumu amesema wanatafuta rekodi za uzao kubaini uhusiano wa sharon mathias na melon lutenyo.

Kwingineko

Huenda usajili wako wa kadi za simu za rununu utafutiliwa mbali iwapo hutojisajili katika mfumo wa Huduma Namba.

Ni kauli ya mamlaka ya mawasiliano nchini CA kwenye "Kikao Kikuu" cha kukusanya maoni kuhusu taratibu za mawasiliano nchini kilichoandaliwa mjini Kisumu.

Mkurugenzi wa mamlaka hiyo Francis Wangusi anasema itakuwa bora kwa kila mmoja kuhakikisha anajisajili katika mfumo huo kabla ya muda ya usajili kukamilika kwa vile baadhi ya watu wamekuwa na mazoea ya kujisajili katika kuchukua kadi zao za simu wakitumia vitambulisho vya watu waliofariki.

Wangusi anasema mfumo huo utasaidia kuleta utaratibu mwafaka utakaozuia usajili wa bandia wa simu ili kuzui aina.

Kwingineko

Usimamizi wa chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali kuu ya Kakamega umepata idhini ya mahakama kuzika miili ishirini ambayo haijatambuliwa na kuchukuliwa na wanafamilia

Msimamizi wa chumba hicho Mustafa yusuf amesema miili hiyo inaleta msongamano na pia kuhatarisha afya ya wahudumu chumbani humo.