Kama Hujui Umri Wa Mwanadada Tazama Kisigino - Arocho

mbuss
mbuss
Kila anapo chukua usukani ndani ya Radio Jambo, iwe ni wakati wa kipindi cha Weekend Warm up au ni katika safu ya utangazaji kabumbu, mtangazaji mashuhuri nchini, Fred Arocho ni mwingi wa ucheshi na viburudisho kemkem.

Anajulikana sana kwa sauti ya kuvutia, sauti ambayo haitoi nyoka pangoni bali inawatoa mashabiki televisheni na kuwaweka karibu na redio zake kila anaposhikilia kipaza sauti. Kama mwanzilishi wa neno, 'Laduuma' kama njia ya kusherehekea bao, Arocho kweli ana vipawa si haba.

Huku spoti ikiwa ndicho chakula chake cha kila siku, ni nadra azungumzie maswala mengine kama siasa au pia mambo ya mapenzi licha yake kuwa mwenye imani kuu na maswala ya mapenzi na familia.

Basi akiwa katika pilkapilka zake za utangazaji, Arocho aligusia swala la umri wa wanawake ambalo liliwaacha wengi wakitibu mbavu zao kwa kicheko.

Huku akiwa anajibu swali kutoka kwa msikilizaji mmoja kwa jina Maryanne Njoroge, Arocho alieleza kwa ustadi jinsi ya kujua ikiwa mwanadada ni mzee au amekula chumvi nyingi.

"Unaua wanadada huficha na marashi kujipamba nini , wewe angalia tu kisigino, unajua kisigino hata upake mafuta bado inaparara tu, wewe tizama kisigino hata upake mafuta bado inaparara tu. We tizama tu kisigino itakuambia kama amepiga thelathini hata ukiweka mafuta kilo kumi bado inaparara."

Alifichua Arocho huku akiongeza kuwa ukitaka kujua umri wa mwanadada usimuulize, we jifanye tu kuna kitu umeangusha halafu chungulia kwani hata kisigino kioshwe na maji ya chumvi na maji moto haking'ari.

Skiza uhondo uliomuacha mchanganuzi Fred Ambani akibubujikwa na machozi.