church

‘Kama hukuja kanisa tuma sadaka kwa mpesa’ Pastor atengeza kundi la whatsapp la waumini wake wote!

Mhubiri mmoja mmoja wa kanisa la   The blessed   Chosen huko Bomet ameamua kutengeza kundi la whatsapp la waumini wake wote kwa lengo la kuhakikisha kwamba kila mmoja analipa sadaka licha ya kukosa kwenda kanisani .

‘Its over!’ Kipusa mkenya aachana mpenzi wake mzungu kwa hofu ya coronavirus

Mhuburi huyo amesema kwa sababu ya agizo la serikali kuwazuia  watu kukongamana makanisani , lazim kila muumini ahakikishe kwamba anatuma sadaka yake kila jumapili endapo haitawezekana watu kwenda kanisani. Josephat Korir ameandika majina ya wote waliotuma  sadaka zao jumapili iliyopita na kuwataka wale ambao hawakuenda kanisani kutuma pesa hizo kwa nambari yake . Hatua hiyo imewashangaza waumini wake ambao baadhi yao wametoka kwenye kundi hilo la whatsapp.

‘Nililala na mamangu wa kambo kumuadhibu babangu’ Dunia ina mambo

Katika ujumbe wake mkali kuhusu umuhimu wa kutoa sadaka ,Korir alionya kwamba watakaokosa kutoa michango yao wasilitarajie kanisa lake kuwapa usaidizi wowote au kujihusisha na mambo yao kama vile harusi ,maazishi na kubatizwa . wengi walionekana kupuuza tisho lake  huku wakisema wako tayari kulihama kanisa hilo kwani makanisa ni mengi .

‘Walitoroka na pesa za harusi , coronavirus ilipofika’

Korir  katika ujumbe wake alisema sadaka ni muhimu ili kuendeleza oparesheni za kanisa lake na waumini walifaa kutii ushauri wake .Wengi  katika sehemu hiyo wanangoja kwa hamu kuona mambo yatakuaje katika kanisa hilo wakati tutakapomaliza vita dhidi ya virusi  vya Corona .

 

Photo Credits: Internet

Read More:

Comments

comments