Waiguru ni msafi! Kamati ya seneti haijampata na hatia

Ebb7ACDWsAEsaPc.jfif
Ebb7ACDWsAEsaPc.jfif
Kamati ya maseneta 11 iliyobuniwa kuangazia mchakato mzima wa kutimuliwa kwa gavana wa Kirinyaga Ann Waiguru haijampata na makosa yoyote.

Kamati hiyo iliyokuwa inaongozwa na seneta wa Kakamega Cleophas Malala imesema kuwa, wawakilishi wa kaunti ya Kirinyaga hawakuwasilisha ushahidi wa kutosha dhidi ya Waiguru .

Kulingana na kamati hiyo, bunge la Kirinyaga halikuwasilisha ushahidi unaoguzia maswala yanayomhusisha Waiguru na ufisadi na hivyo wameitaka idara ya maadili na kupambana na ufisadi EACC pamoja na DCI kuanzisha uchunguzi dhidi ya ufisadi katika kaunti hiyo.

Waiguru alikuwa ametimuliwa na wawakilisha wa kaunti ya Kirinyaga kwa madai ya matumizi mabaya ya ofisi,utaoji zabuni kwa kampuni zenye uhusiano na familia yake pamoja na madai mbali mbali ya ufisadi.

MHARIRI: DAVIS OJIAMBO