'Kanisa langu ni la wezi na kahaba,' mchungaji Francis Maina

francis maina
francis maina
Mchungaji Francis Maina, ndiye aliyekuwa mgeni wetu siku ya Ijumaa katika kipindi cha Ilikuaje, naye Massawe Japanni.

Mchungaji huyu ambaye alikuwa amehukumiwa kunyongwa mwaka wa 1992, kufuatia wizi alinusurika kufuatia msamaha wake rais Moi mwaka wa 1993.

Kufuatia hayo yote bwana Francis, sasa amefungua kanisa kwa jina,World Mission Centre, Gachie, ambalo linakaribisha wahalifu na pia ambao wanatumia mihadarati.

Anasema kuwa aliamua kuwapa wahalifu fursa kwani ni vigumu sana wafungukie yeyote kuhusu maisha yao. Isitoshe, vijana sasa hivi haswa wanaotumia madawa za kulevya wametengwa sana na jamii.

Nguzo ambazo zinasimamisha vijana ni familia, serikali na pia kanisa. Pale Gachie kuna vijana wamekataliwa hata na kanisa na tukafikiria njia za kufikia wale vijana ambazo sio rahisi. Alisema Francis.

Katika kanisa letu, sisi hukutana kila Jumanne saa nane na tunawazungumzia wale watu na pia tunawapa chakula, ambao ni wanawake na wanaume.

Ile kuzungumza nao wakaanza kuita wenzao ili pia wabadilike.

Frank anadai kuwa alianza uhalifu akiwa kijana mdogo wa miaka 16, uhalifu ulioanzia akiwa katika michezo yake ya kamari pamoja na rafiki zake.

Walianza wizi wa kuibia watoto wa wahindi baiskeli na kuziuza, fedha ambazo walikuwa wanatumia kucheza kamari.

Baada ya mda tamaa ya fedha iliongezeka na wakaanza kuiba vipuli vya magari, kisha kuhitimu kuiba magari huku akitumiwa silaha na nikatika pilka-pilka hizo ambapo alipigwa risasi mguuni kabla ya kuhukumiwa kinyongo.

Sikuzaliwa nikiwa nachuchumaa kwani hayo ni mazaliwa ya uhalifu. Siku moja tulienda kuiba pesa Guru Nanak na kwa bahati mbaya tukashika gari ambayo sio na katika ile hali ya kupigana na polisi nikapigwa risasi mguuni.

Nilikutana na jaji Ben Chunga kortini mara mbili na mara ya tatu ndipo alinihukumu kinyonga kwani alikuwa ameniahidi kuwa akinipata kwa mara ya tatu atanihukumu kunyongwa.

Bwana Francis ambaye amefungwa katika jela kadhaa nchini zikiwemo; Shimo la Tewa, Naivasha na pia Kamiti, alikuwa kiongozi wa majambazi ambao walihangaisha watu mtaa wa Eastleigh kwa miaka mingi.

Cha kushangaza ni kuwa yeye na wenzake waliwahi tekeleza wizi wa fedha katika benki ya Baroda mara tatu bila kushikwa.

Mara ya tatu ndipo walipo fumaniwa na polisi katika eneo la Globe Cinema ambapo wenzake waliuliwa lakini alifanikiwa kupotea baada ya kujificha ndani mwa gari la polisi na kutorokea Ngara.

Aliongeza kuwa hapo ndipo alipoamua kubadilisha mienendo yake.

Kuna siku tuliiba Bank of Baroda, Tom Mboya, milioni nne, isitoshe tuliiba mara tatu na nashuku hilo ndilo lilipelekea benki hiyo kufungwa.

Tulipoiba mara ya tatu nilishikwa na nikafungiwa Nyayo House kwa mwezi mmoja, na mle ndani hakukuwa na mwangaza, nilikuwa nalalia maji na chakula sikuwa napewa kila siku. Jeans niliyoingia nayoilitoka ikiwa kaptula baada ya kuliwa na panya.