Katibu msimamizi Charles Hinga aongoza hafla ya kusafisha miji

EW1vkSHWsAAegl8
EW1vkSHWsAAegl8
NA NICKSON TOSI

Baada ya rais Kenyatta kudai kuwa serikali itaanza mpango wa kuwaajiri vijana watakaofanikisha usafi wa miji nchini,katibu katuko idara ya nyumba bora na miundo msingi  Charles Hunga amezindua rasmi mchakato huo hii leo huku maelfu ya vijana wakijitokeza kusajiliwa.

Mradi huo unapania kubuni nafasi za ajiri kwa vijana katika mitaa ya mabanda na maeneo mengine nchini .

Katika hotuba yake rais Kenyatta alisema kuwa vijana ndio watakaokuwa wakwanza kusajiliwa kwa mradi huo ulionzishwa na serikali kutokana na idadi ya baadhi yao kukosa ajira.

Katika kaunti ya Mandera na ambayo imeathirika pakubwa na virusi vya Corona ,shughuli hiyo imeanzia mji mkuu wa Mandera .

Vijana 6000 kusajili katika kaunti ya Mombasa