Kenya ina maabara mawili ya kupima virusi vya Corona

Kenya sasa ina maabara mawili kwenye kituo cha kitaifa cha homa na katika taasisi ya uchunguzi wa kimatibabu nchini KEMRI ambayo yanaweza kutumika kupima virusi vya Corona.

Serikali inasema sasa haitahitaji kupeleka sampuli zake kufanyiwa uchunguzi nchini Afrika Kusini.

Hata hivyo mtu yeyote ambaye ametembelea nchi ya uchina hivi majuzi na ana dalili zozote za ugonjwa wa kupumua ameshauriwa kumwona daktari.

Virusi hivyo kufikia sasa vimesababisha vifo vya zaidi ya watu elfu moja mia tatu tisini 1390 kote ulimwenguni huku wengine zaidi ya elfu 50 wakiambukizwa.

Hayo yakijiri, kuwasaidia wale wanaowahudumia watu wanaoishi na ulemavu kunaweza kuwapunguzia mzigo huo na kuwazuia kuwa hoi kabisa.

Mshauri James Mbugua anasema wahudumu hao wanapokosa kupewa usaidizi wengi wao huhuzunika kwani wanahisi kana kwamba wamelemewa pia.