Kenya kupiga marufuku utumizi mmoja wa chupa za plastiki - 2020

Chupa za plastiki sasa hazitaruhusiwa katika baadhi ya maeneo humu nchini. Rais Uhuru Kenyatta alitangaza marufuku dhidi ya utumizi mmoja wa plastiki kwenye maeneo yanayolindwa humu nchini.

Marufuku hiyo iliyotangazwa Siku ya Mazingira Ulimwenguni inahusisha mbuga za kitaifa, misistu na fuo itaanza kutekelezwa kuanzia tarehe 5 Juni 2020.

Marufuku hiyo imetangazwa miaka miwili baada ya kuharamishwa kwa utumizi, utengenezaji, na uuzaji wa plastiki zenye madhara kwa mazingira, mifuko ya plastiki na vifaa vya kupakia.

"Mnavyofahamu, Kenya ni mwenyeji wa mpango wa mazingira na imeendesha kampeini ya maendeleo endelevu. Kutokana na jitihahada hizi, miaka miwili iliyopita tulipiga marufuku utumizi, utengenezaji na uuzaji wa plastiki zenye madhara kwa mazigira, mifuko ya plastiki na vifaa vya kupakia," kasema Rais.

"Kwa kutegemea haya, hii leo tunatangaza marufuku nyingine dhidi ya utumizi mmoja wa plastiki katika maeneo yetu yote yanayolindwa zikiwemo: Mbuga za kitaifa, fuo, misistu na maeneo ya hifadhi kuanzia tarehe 5 Juni, 2020," kaongezea Rais.

Pia soma:

Rais alitoa tangazo hilo alipohutubia kikao cha kongamano linaoendelea la 2019 katika Jumba la Mikutano la Vancouver nchini Canada.

Rais alipongeza Canada kwa kuongoza juhudi za kuendeleza haki za wanawake kupitia Sera ya Kigeni ya Kimataifa Kuhusu Wanawake akisema mbinu hiyo inabadilisha mtizamko wa ulimwengu kuhusu nafasi ya haki za wanawake kuamabatana na maswala yote katika jamii.

Pia soma:

"Kwa ulimwengu kustawi, hakikisheni maisha ya thamani kwa raia, uongozi bora unaoitikia matarajio ya raia wake, sharti la kutegemea raia wote, wala sio kutegemea takribani nusu ya raia wake," kasema Rais.