Kenya yabadili hatua yake na kuruhusu ndege kutoka Uingereza na Amerika kutua nchini

kibe-macha
kibe-macha

Taifa ;la Kenya sasa limebadili hatua yake ya kuzuiya ndege za mataifa manane yakiwemo Amderika na Uingereza kutua nchini licha ya kurejelewa kwa shughuli za usafiri Jumamosi.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na halmashauri ya usafiri wa ndege nchini KCAA,mataifa mengine manane yaliongezwa katika orodha ya mataifa kumi yaliyokuwa yameruhusiwa kuanzisha usafiri wa ndege moja kwa mjoa hadi nchini.

Kutokana na hatua hiyo sasa,mataifa ya Amerika,Uingereza Milki za kiarabu UAE,Italia,Ufaransa,Ujerumani ,Uholanzi na Qatar yote yamejumuishwa kwenye orodha hiyo na kufikisha mataifa 19 sasa yanayoruhusu masharika ya ndege zake kutua nchini.

Waziri wa Uchuguzi nchini James Macharia alitangaza mataifa 11 ambayo yangehudumu nchini japo hakusema iwapo wasafiri kutoka mataifa hayo wangewekwa chini ya karantini kwa kuwasili.

Licha ya mataifa hayo kuongezwa hadi kufika 19,taifa jirani la Tanzania halijajumuishwa katika mataifa hayo ,ikiashiria wazi mgogoro uliopo wa kidiplomasia baina ya mataifa hayo mawili.

Shirika la ndege la KQ nchini lilirejelea shughuli zake za kawaida Jumamosi na kuanzisha safari za moja kwa moja hadi kwa mataifa 30 kwa mara ya kwanza tangu kusitishwa kwa usafiri wa angani mnamo Machi  mwaka huu bnaada ya kuripotiwa kwa virusi vya corona.