Kenya yafikisha siku ya 100 tangu kisa cha kwanza cha Covid-19 kuripotiwa huku visa 260 vipya vikisajiliwa leo

Serikali imeadhimisha siku 100 tangia kisa cha kwanza cha virusi vya corona kuripotiwa, mnamo tarehe 13 Mechi, 2020.

Akipeana ripoti kuhusu jinsi hali ilivyo sasa hivi, waziri wa afya Mutahi Kagwe alisema kuwa serikali imefanikiwa kuzuia virusi hivyo kusambaa zaidi tangia kisa cha kwanza.

Waziri pia alisema kuwa serikali itaongeza jitihada ili kuongeza vifaa zaidi vya kufanyia vipimo katika majuma yajayo.

Kagwe alisema kuwa safari haijakuwa nyororo kwani watu 123 tayari wamepoteza maisha yao.

Katika kipindi cha masaa 24 yaliyopita, Kenya imeandikisha visa 260 vipya, hiyo ikiwa idadi ya juu zaidi kuandikishwa tangia kisa cha kwanza kuripotiwa.