Kesi dhidi ya Julius Malema yaahairishwa

Kesi ya ufisadi inayomkabili kiongozi wa upinzani nchini Afrika Kusini Julius Malema, imeahirishwa hadi Agosti mwaka ujao.

Kesi hiyo ilitarajiwa kuanza hii leo lakini wakili mmoja muhimu hakuwepo.

Kiongozi huyo wa zamani wa kundi la vijana wa chama kinachotawala cha ANC anashtakiwa kwa ulaghai, matumizi mbaya ya fedha na kwa kuuza vitu kimagendo.

Bwana Malema amekanusha makosa yote na kusema kuwa madai dhidi yake yamechochewa kisiasa.

Kwa taarifa kamili soma: http://www.bbc.co.uk/swahili/habari/2014/09/140930_malema_korti