Kifo hakina huruma: Vile wachezaji Joan na Valerie walifariki - Willy Paul

Si jambo la kawaida kumpoteza rafiki wa karibu ama rafiki umpendaye, ni kumbukumbu zitakazo kuwa katika akili ya msanii Willy Paul kwa kuwapoteza wachezaji wa nyimbo zake kwa njia tofauti.

Akiwa katika mahojiano, Willy alifunguka na  kueleza vile vifo vya Valerie na Joan viliweza kumpiga butwaa na kuachwa katika mshtuka mkubwa baada ya kila mmoja kufariki baada ya wiki.

Aliweza kupokea simu isiyofurahisha kuwa Joan ameweza pia kuaga dunia, kupitia ajali ya barabara aliweza kufichua na kusema kuwa dereva ambaye alikuwa amembeba Joanne aliweza (overtake) mahali ambapo palikuwa pabaya kisha kukumbuka wakati wa mwisho.

Alisema kuwa matokeo ya gari hiyo iliweza kukimbia mbali hadi kwenye mti,gari hiyo iliweza kugonga mti mahali Joan alikuwa ameketi kisha akapata majeraha mabaya ya kichwa na kwenye shingo.

Willy alimaliza moyo wake ukiwa umevunjika na kusema ,"Alikufa papo kwa hapo."