Kifo! Kifo! Mulamwah aomboleza kifo cha ghafla cha mwigizaji mashuhuri

John Simiyu Masinde anayejulikana kwa jina maarufu la John Gift ameaga dunia. Alikuwa mwanzafunzi wa mwaka wa nne kwenye chuo kikuu cha Eldoret.

Chale huyu ambaye alikuwa nafanya filamu za ucheshi kwa lugha ya kiluhya alikufa ghafla. Mwandani wake, Mulamwah ndiye aliyevunja habari hizo za huzuni kwa mashabiki wa John Gift.

''Maisha yanaweza kuwa katili nyakati zingine 😭. Mcheshi JOHN GIFT ameaga dunia. Chanzo cha kifo chake bado si dhahiri lakini alikuwa kwenye chumba cha wagonjwa hali mahututi kabla atamkwe kuwa ameaga mapema leo (Juni 2),'' Mulamwah alisema.

Kulingana na sources, John Gift alikuwa anavuja damu kutoka kwa pua na mdomo wakati alipokuwa anakimbizwa hospitalini na alipelekwa kwenye chumba cha wagonjwa hali mahututi.

Familia yake ilijuzwa kuwa alikuwa anapigania maisha yake hospitalini na baada ya masaa machache akakata roho.

Mulamwa aliongeza,''Nilifanya naye video yangu ya mwisho Alhamisi tarehe thelathini mwezi wa Mei na hali yake ilikuwa njema. Lala salamu ndugu. Endelea kung'aa. Habari zaidi kuhusu kifo chake cha ghafla itawasilishwa. Ni pigo kubwa kwenye idara ya ucheshi, alikuwa mtu mwenye ubunifu. Lala salama Johnny.''

Wacheshi wengine waliopigwa na mshtuko kuhusu kifo hicho cha ghafla walituma rambirambi zao.

Terence Creative ambaye anajulikana kama mhusika mcheshi Kamami aliandika, ''Waaaaaa yahuzunishaaa alale salama .''

Mtoto wa Akothee, Fancy Makadia aliandika, ''LALA SALAMA.''

Mwigizaji Pascal Tokodi aliomboleza na familia hiyo akisema, ''Roho yake ilale pema , pole ndugu🙏''

Mcheshi Kartelo aliongeza , ''Lala salama mwanajeshi 🙏 angaa mwangaza njiani.''

John Gift alijieleza kwenye mtandao wake wa Instagram kama mtu ambaye ''alichukulia uimbaji na ucheshi kama zawadi kubwa kutoka kwa Mungu hivyo jina John Gift.''

Tazama moja wapo ya video zake ambapo hajafanya na kiluhya

Mashabiki wa John Gift walitoa rambirambi zao. Tazama baadhi ya jumbe zao.

lee_chiquita_hermosa: Just as I thought we’ve made it to the industry, then boom death happened. John, you’ve left without knowing how happy you made us. I’m confused. I don’t know if I should laugh at your jokes or cry that you’ve left us. In God’s hand, we rest you😢#restpeacefully 🙏💔

lilianwekesa: Just when I had started following you a month ago now I can’t enjoy more of your funny creativity…😭😭😭Death is so cruel

rawbeanhd: What a painful death… God has the reasons as to why everything happens.