KINANGOP: Ajuza wa miaka 85 adhulumiwa kabla ya kuuawa

Wakazi wa eneo la Engineer katika mji wa Kinangop waliamka kwa mshtuko baada ya nyanya wa miaka 85 kupatikana akiwa amedhulumiwa kabla ya kuuawa.

Wakati wa tukio ilo la kushangaza katika kijiji cha Kahuru, idadi iya majambazi isiyojulikana ilitoweka na bidhaa za nyumba huku polisi wakiingilia kati kuchunguza tukio hilo.

Kulingana na OCPD wa Engineer, Charity Dorcas, nyanya huyo alikuwa amewasili nyumbani kwake kutoka Nairobi na alikuwa anajitayarisha kufanya shughuli zake za kilimo.

Alisema kwamba hapo awali mwanamke huyo angekuja mara moja kwa mwezi kulipa wafanyikazi wake na kusimamia kile kinachoendelea katika shamba lake.

“We suspect that the suspects thought the woman had cash and in the robbery process they also sexually abused her but it’s a matter of time before we catch up with them,” alisema.

Mzee wa kijiji hicho, Joel Kimani alisema kuwa tukio hilo ni la kushtua na akawasihi polisi kuhakikisha wale walio tekeleza unyama huo wamekamatwa.