'Its over!’ Kipusa mkenya aachana mpenzi wake mzungu kwa hofu ya coronavirus

Kenya ina mambo ,lakini cha msingi  uhai ni kitu muhimu sana .  Huko Nyali ,virusi vya corona vimewafanya wawili waliopendana kwa mwaka mmoja kuachana ghafla huku mwanana  Mkenya akikataa kumkaribia mchumba wake mzungu raia wa  Udachi aliyewasili nchini mwisho wa mwezi jana wakati janga la corona lilipokuwa limeanza kuyatesa mataifa mengi ya bara ulaya .

Mrembo huyo ambaye ni  model alikutana na  mzungu katika  tamasha moja ya utamaduni mjini Malindi mwaka  mwanzoni mwa mwaka jana na walikuwa wamepiga kasi sana kuhusu maisha yao ya baadaye na hata walikuwa wamezungumza kuhusu ndoa . Lakini mwanamme huyo alisafiri kwenda Holland  mwezi januari na wakati huo virusi vya Corona vilikuwa tu vikiripotiwa kukithiri nchini China .  Visa  vya ugonjwa huo vilipoanza kuripotiwa barani ulaya ,mzungu alimua kurejhea Kenya haraka ili awe na mpenzi wake na asiweze kufungiwa nje ya nchi endapo janga hilo lingefika afrika .

Kitu ambacho hakujua ,ni kwamba watu wengi walikuwa wameanza kugundua kwamba wengi wa waliosafiri nje ya nchi ndio waliokuwa wkairejea wkiwa na virusi hivyo na maskini msichana wa kikenya alikuwa ashaamua kwamba kamwe hatotangamana na  mpenzi wake huyo zmungu atakaporejea . Alichukua vitu vyote katika nyumba ya kifahari mtaani Nyali na kuvihamisha hadi nyumba nyingine aliyokodisha karibu na Bamburi .Mzungu alipofika uwanja wa ndege ,alishangaa kwamba mpenzi wake hakuwepo kumpokea . Alipojaribu kumpigia  hakushika simu yake na badala yake alimtumia ujumbe kwamba hataki tena uhusiano huo akihofia kuambukizwa virusi vya corona .Hali imefanywa kuwa mbaya kwao kwa sababu mzungu ana umri wa juu kumliko na hivi  inasemekana virusi hivyo vinawashambulia kwa haraka watu wa umri wa juu kuliko wenye umri mdogo .

Akifikiri  ni utani  mzungu kazungushwa Mombasa nzima akimtafuta mrembo huyo  hadi akachoka na  kulazimika kwenda hotelini ili aanze tena kujitayarisha kurejea kwao.Akingoja kurudi Holland ,virusi vya Corona vikaripotiwa Kenya na baadaye serikali kupiga marufuku safari za ndege .Jamaa hajui atarejea vipi kwani ana hadi  jumatano tarehe 25 kuondoka Kenya kwa mujibu wa agizo lililotolewa na serikali ya Kenya .