Kisa cha kutatanisha kisiwani migingo

Hali ya wasiwasi na  biwi la simanzi imetanda katika kisiwa cha Migingo kwenye kaunti ya Migingo baada ya kuuawa kwa hali isiyoeleweka kwa mfanyibiashara kutoka nchini Uganda usiku wa kuamkia leo.

Mwenyekiti wa ufuo wa kisiwa cha Migingo John Obunge alisema kuwa mwili wa mfanyibiashara huyo  Kennedy Mugwaru wa kuuza maji ulipatikana ukielea kwenye maji bila ya kuwa na  masikio,mdomo kukatwa na  mapua na  kudaiwa kuuawa kwa minajili ya kufanyia viungo hivyo uchawi wa kusaidia katika kuboresha kazi ya uvuvi.

Obunge alidai kuwa mfanyibiashara huyo aliripotiwa kutoweka siku tano zilizopita na  mwili wake kupatikana ukiwa umekatwa baadhi ya viungo ikiwemo sehemu nyeti za mwili kwa kufanyia tambiko la kuwezesha kuvua samaki wengi.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha maiti cha hospitali ya Bukwe huku polisi kutoka Nyatike wakiendelea na uchunguzi zaidi kuhusu kisa hicho.