Kiunjuri mashakani kuhusu malipo ya shilingi bilioni 1.8.

Wizara ya Kilimo ilitoa shilingi bilioni 1.8 kutoka hazina ya hifadhi kitaifa ya chakula kinyume na sheria bila idhini ya bodi inayohusika, hatua ambayo imemuweka waziri wa Kilimo Mwangi Kiunjuru mashakani.

“Ufichuzi wako kuhusu malipo ya shilingi bilioni 1.8 kutoka hazina ya hifadhi ya kitaifa ya chakula nchini kwa kampuni ya Commodity House bila idhini ya bodi ilikuwa kinyume na sheria,”Mwenyekiti wa bodi hiyo Noah Wekesa alisema katika barua ya Julai, 9.

Malipo hayo yalidaiwa kulipa deni la mahindi yaliyoagizwa mwaka 2017. Kiunjuri jana aliambia bunge kwamba Commodity House inadai serikali shilingi bilioni 3.6. Hata hivyo wabunge, wengi wao kutoka maeneo yanayokuza mahindi walidai kwamba malipo hayo yalikuwa ya kuagiza mahindi ambayo bado hayajawasilishwa nchini.

Habari zaidi:

Katika stakabadhi za msajili wa makampuni nchini Commodity House inamilikiwa na wakurugenzi wanne. Wanne hao ni Richard Ethan Ndubai, Stehen Cheruiyot Kositany, Daniel Mburu Wainaina na Reginald Willingston Karanja.

Habai zaidi:

Kufuatia ufichuzi huo, wabunge jana walimtaka Kiunjuri na katibu wa kudumu wa ustawi wa kilimo Hamadi Boga kujiuzulu ili kutoa nafasi kufanyika kwa uchunguzi wa kina. Wabunge hao wanamtaka Kiunjuri kung’atuka ofisini na walitishia kuwasilisha bungeni hoja ya kutokuwa na imani naye wiki ijayo ili kumshinikiza aondoke ofisini.

Kiunjuri ambaye alishikilia msimamo wake kuhusu uagizaji wa mahindi, kinyume na msimamo wa bodi ya hifadhi ya kitaifa (SFR) - ambayo inajukumu la kuishauri serikali kuhusu hali ya hifadhi ya chakula nchini – alipuuzilia mbali madai ya ukiukaji wa sheria katika malipo hayo ya shilingi bilioni 1.8 .