Kizaazaa Huku Patanisho Ikigeuka Kuwa Tenganisho (AUDIO)

Ney wa Mitego
Ney wa Mitego
Asilimia themanini ya vitengo vya patanisho huishia na furaha baada ya waliokosana huku wakiwa mandugu, wapenzi na hata pia wakwe kusameheana.

Asilimia ishirini iliyobakia aidha huishia kwa; Waliokosana kukosa kuelewana au mitambo inaleta shida hapa na pale au pia anayeombwa msamaha kukataa kushika simu zetu.

Basi hivi majuzi patanisho iligeuka kuwa tenganisho baada ya mwanadada aliyeleta patanisho kukutana na pingamizi kuu kutokana na jamaa aliyekuwa bwanake, kisa na maana kuwa aligeukia tabia za ukahaba na basi kuamua kurudiana na mkewe ambaye alianza tabia za wanaume hapo awali, kwa madai kuwa alifanya kosa mara moja na isitoshe ndie mama wa watoto wake.

Faith 28, aliomba apatanishwe na bwanake bwana Magana mwenye umri wa miaka 43, ambaye walikosana takriban mwezi mmoja uliopita.

"Mimi ndiye niliyemkosea nikamtumia ujumbe nikisema "Kama hushiki simu yangu yale unayoyafanya pia mimi nitafanya." Na hapo alikasirika na haniongeleshi. Mimi nilifikiria pengine ana mwanamke, sahizi huwa ananikumbusha yale na sikuwa namaanisha kwani ilikuwa wivu wa mapenzi." Alijieleza Faith akisema kuwa bwanake huwa harejei nyumbani na hulala ndani ya gari kazini.

Wawili hawa wamekaa kwa ndoa kwa mwaka mmoja pekee lakini hawajaliwa mtoto kwani Faith anashida ya uzazi lakini bwanake alikubali kumpenda alivyo. Aliongeza kuwa yeye ndiye hulea watoto wake wa kambo.

Alipopigiwa simu, bwana Magana ambaye ni dereva wa masafa marefu alisema kuwa hii sio patanisho labda iwe tenganisho akidai kuwa siku moja akiwa Mombasa alikutana naye katika gari lingine eneo la Sultan akidai kuwa ana shughuli kwa shamba moja alilokodisha.

"Hapo nikaona anataka tu kubebwa na malori kwani ukibebwa na lori utapewa chakula bure na vinywaji bure na dereva ataburudika nawe. Ukimpa fedha za basi anajificha anapanda kwa lori na hapo nikaona hizo tabia siwezani nazo na nikaamua kurudiana na mke wa kwanza kwani alikosea vilevile lakini wana watoto pamoja."

Alijieleza bwana Magana akidai kuwa "Kuna siku alinieleza kuwa nikienda safari za mbali anaweza safiri na arudi kabla mie nirudi. Mwanadada huyu sio muaminifu na nina uhakika kwa kurudiana naye ni kujitafutia ugonjwa."

Bi Faith naye alikiri kuwa bwana Magana alikuwa tu anamchafulia jina na kuwa hakumpendea mali yake. "Hakuna kitu mbaya nitasema juu yako kwani nilikuwa nakupenda."

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be