KNEC: kemikali zilizotumika katika mitihani ya KCSE haina sumu

Serikali imekataa ripoti kwamba kemikali zilizotumiwa wakati wa mtihani wa KCSE wiki iliyopita zilikuwa na sumu.

Baraza la kusimamia mitihani nchini KNEC wamesema kuwa kemikali xylene, bromine, na calcium hypochloride ni miongoni mwa vitu vilivyoidhinishwa kwa matumizi ya maabara shuleni.

 KNEC  walikuwa wanajibu ripoti iliyoibuka katika mitandao ya kijamii kuwa baadhi ya walimu waliugua baada ya kuvuta pumzi ya kemikali wakati wa mtihani uliofanyika siku ya alhamisi.

Mercy Karogo ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa shirika la mitihani alisema kuwa baraza hilo limeelezea tahadhari za usalama wakati wa kushughulikia vitu vyenye hatari shuleni.

Mercy aliongeza kuwa hakuna kisa kimeripotiwa kuhusu kuugua kwa walimu au hata wanafunzi.

Jumuiya ya walimu KUPPET imeibua wasiwasi juu ya athari ambayo kemikali hizo zinaweza leta kwa walimu na wanafunzi.

KUPPET ilieleza kuwa shule nyingi haziwezi kuhakikisha usalama wa wanafunzi na walimu wanaoshughulikia kemikali hizo hatari kwenye maabara isiyo na rasilimali.

Belio Kipsang ambaye ni katibu katika wizara ya elimu alisema kuwa kemikali hizo ni zile zile wanafunzi wamekuwa wakitumia wakati wa mazoezi wa kemia katika masomo ya kawaida.