Kocha wa Gor Mahia, Hassan Oktay ajiuzulu rasmi

hassan oktay
hassan oktay
Kocha wa Gor Mahia Hassan Oktay amejiuzulu rasmi kama meneja wa klabu hiyo. Kwa mujibu wa tovuti ya klabu hiyo Oktay ameiomba Gor kumwachilia kutoka kwa mkataba wake ambao ulikua ukamilike baadae mwaka ujao.

Tangazo hili limepokelewa kwa mshtuko kwani raia huyo wa Uturuki alikua ameomba muda kusafiri nchini mwake kwa masuala ya kifamilia. Oktay hata hivyo ameishkuru klabu hiyo kwa kumpa fursa ya kusimamia magwiji hao wa soka nchini.

Mahakama ya kusuluhisha mizozo ya spoti hii leo inatarajiwa kutoa uamuzi, kuhusu kesi inayopinga hatua ya Athletics Kenya kuwapiga marufuku kuiwakilisha nchi, wanariadha ambao awali walitumikia marufuku ya kutumia dawa zilizoharamishwa.

Kesi hiyo imewasilishwa na mwanariadha Ferdinand Omanyala, ambaye alimaliza marufuku yake mwaka uliopita. Mahakma hiyo iliiagiza AK kumruhusu kushiriki majaribio ya All African Games ambayo alifuzu, lakini hana uhakika iwapo ataruhusiwa kuiwakilisha Kenya.