Korti yaachilia huru ndugu wawili walioshtakiwa kuua

Korti mmoja mjini Eldoret iliwachilia huru ndugu wawili ambao walikuwa wametuhumiwa mauji baada ya hakimu Stephen Githinji kukasirishwa na uhamisho wa kesi yako na afisi ya DPP kwa miaka mitano iliyopita.

Hakimu Githinji aliwaachilia washukiwa hao ambao walikuwa wamefungwa miaka mitano jela bila kesi yao kuskizwa hadi mwisho.

Misiko na nduguye Geoffrey Misiko walishtakiwa kwa kumuua nduguye Benson Misiko Julai 12 mwaka wa 2014 katika kijiji cha Murram, jimbo la Lugari, kaunti ya Kakamega.

Huku akitoa uamuzi uliowashangaza wengi na kuwaachilia washukiwa huru, aliilaumu afisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma kwa kukosa kuonesha nia ya kushtaki kesi hiyo hadi mwisho kama inavyohitajika.