KPLC: Wakurugenzi 5 Wa Kenya power wajiuzulu +Podi Maalum kuhusu mahangaiko ya wakenya kupata huduma za umeme

KPLC
KPLC
Bodi ya kusiamamia Kampuni ya kutoa huduma za umeme nchini Kenya power imetangaza  kujizulu wa wakurugenzi huru 5  kutoka kampuni hiyo.

Kupitia kwa taarifa iliyotumwa kwa umma, kampuni hiyo imetangaza kujiuzulu kwa wakurugenzi hao  Adil Khawaja, Kairo Thuo, Wilson Kimutai, Brenda Kokoi  na Zipporah Kering.  Bodi ya kampuni hiyo imewashukuru kwa huduma zao na kuwatakia heri katika shughuli zao  zinazofuata.

Sikiza podi hii kuhusu masaibu ya wakenya wengi kutokana na utendaji kazi wa kampuni hiyo.

&t=405s

KPLC imejipata ikipondwa na wanangwa na lalama za  udhaifu mkubwa katika utendakazi wake kwa ajili ya uhaba wa nguvu za umeme na kukatizwa kila mara kwa huduma za umeme hatua inayowasababishiwa watu wengi hasara ya mamilioni ya fedha. Licha ya kuwa kampuni pekee inayotoa huduma za umeme, Kenya  Power imekuwa ikiripoti kupata hasara katika matokeo yake ya kifedha, huku visa vya ufisadi na uporaji wa fedha za umma vikilipukia kutoka  kwa wasimamizi wa kampuni hiyo .