Kupoteza Simu Kanisani Ni Kama Kupoteza Sadaka Kwa Bar, Gidi Ampasha Ghost (AUDIO)

mentorship 1
mentorship 1
Sote twamjua bwana Ghost Mulee na ucheshi na talanta ya kuburudisha waskilizaji wa Radio Jambo kila uchao.

Pia tunafahamu uwezo wake wa kujitoa au kujinasua kwenye masaibu haswa kila anapochelewa kufika kazini huku akiwa mwingi wa vijisababu, ujanja ambao umemwezesha kuepuka 'adhabu' ya mdosi wake bwana Gidi huku akiwaacha wengi wakiangua vicheko.

Mojawapo ya vijisababu anavyotembea navyo ni; Gurudumu la gari liliharibika, alimpata nyoka akiwa amevingira gurudumu la gari lake, mara saa yake ya kengele haikuitana.

Basi leo bwana Mulee aliingia kazini mda mchache akiwa amechelewa na kama ilivyo ada, mwenzake Gidi hakuchelewa kumuanika hewani huku akifurahishwa na jinsi alivyo nyemelea studioni.

"Mwenzangu bwana Mulee naona unaingiaingia unanyemelea kama panya anaye tafuta... ama ni paka anayetafuta panya? Nimeona vile umenyemelea uko karibu kuniambia Gidi si nilikua hapa." Gidi alimkaribisha Ghost.

Huku akifahamu fika kuwa bwana Mulee alisafiri hadi maeneo ya Machakos ambapo kulikuwa na mchuano wa Harambee Stars na DRC Congo, Gidi alijijazia kuwa huenda bwana Mulee alishindwa kuamka, na hapo ndipo Mulee alifichua yaliyotendeka.

"Ah ndugu yangu mimi nimeamka nafikiri ni Saturday. Kuchungulia naona leo ni lini jameni? Sasa ndio nikakumbuka ah jana nilikuwa Machakos ilikuwa Sunday leo lazima niende kazini jameni."

Alijitetea kabla ya kusimulia kuwa alipoteza simu yake kanisani siku ya Ijumaa.

"Wikendi imekuwa bomba, nimekuwa busy na by the way Friday tena nikapoteza simu yangu pale kanisani nilikuwa nimeenda njia ya msalaba pale Queens of apostles Ruaraka sasa sijui simu ilianguka kanisani ndani ama nikitoka na baiskeli yangu nilipoteza simu, nikapoteza miwani yangu."

Alielezea Bwana Mulee. Baada ya mda mchache bwana Gidi bado alikuwa anasumbuliwa na swala hilo na hapo akaamua kumpasha bwana Mulee, kwani bado hakuelewa jinsi unavyoweza poteza simu kanisani huku akilinganisha kisa hicho kama kupoteza sadaka kwa bar.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be