Kutana Na Msanii Reginald Mghanga, Ambaye Ustadi Wake Umewapendeza Gidi Na Ghost

Kwa mda sasa, Usanii nchini umeanza kutambulika kuanzia shuleni hadi kwa wenye wameifanya kuwa taaluma ambayo wanapata mkate wao wa kila siku.

Swala hili ambalo limekuwa tangia miaka ya kale limeimarisha sanaa na tamaduni nchini, na baada ya serikali kuu ya Kenya kuweka sanaa chini ya wizara ya michezo na utamaduni, wasanii wa nyimbo na pia wachoraji kama Reginald Mghanga wamenufaika.

Kutana naye msanii, Reginald Mghanga, mchoraji chipukizi kutoka pwani ambaye kwa miaka mingi sasa amejiimarisha kama mojawapo ya wasanii bora zaidi nchini.

Bwana Mghanga ambaye hufanya michoro ya aina yoyote kuanzia wanyama hadi michoro ya watu, ambayo pia huwa ya kidijitali, ameweza kujipatia riziki yake ya kila siku kufuatia kipawa chake ambacho kimemuezesha kukutana na watu mashuhuri nchini.

Hapo jana tulipata fursa ya kumhoji Reginald ambaye mchoro wake stadi wa watangazaji wa Radio Jambo, Joseph Ogidi na Jacob "Ghost" Mulee wa kipindi cha Gidi na Ghost Asububuhi, uliwapendeza watangazaji hao ambao umaarufu wao umeenea kote nchini.

Lakini je, ni kipi kilicho mpa motisha wa kuwachora watangazaji hao?

"Mimi ni shabiki wa kipindi cha Gidi na Ghost Asubuhi kwani mimi huwaskiza kila asubuhi, na hata kabla ya kipindi hicho kianze mimi kama shabiki wa kandanda nilikuwa shabiki wa Ghost Mulee ambaye alikuwa kocha wa Harambee Stars. Siku moja rafiki yangu akanihamasisha nifanye mchoro wa watangazaji hao."

Alisimulia msanii huyo ambaye alikiri kuwa mchoro huo ambao ulimchukua siku kumi na nne kuukamilisha, utawagharimu kati ya  shilingi elfu ishirini na tano hadi elfu thelathini.

Lakini je fedha nyingi ashawahi pata kupitia usanii wake ni ngapi, na je Gidi na Ghost watauununua mchoro huo?

Pata uhondo kamili katika mahojiano yetu katika kanda ifuatayo.