Kutoka kwa Nameless hadi kwa Nyashinski,'Wasanii walioimba katika harusi ya Bien

bienproposes1
bienproposes1
Msanii wa kundi la Sauti sol Bien alioa mpenzi wa maisha yake Chiki  kwa harusi ambayo ilihudhuriwa na watu zaidi ya mia moja, wawili hao walifunga ndoa kwa njia ya siri.

Hii ni baada ya watu wengi kungoja kwa muda mrefu wawili hao waoane.

Wawili hao walisherehekea ndoa yao kwa kutia saini mkataba wa harusi na kula viapo ijumaa.

"We will not have a white wedding because a white wedding was introduced by the white, and I am not going to follow that since its like colonisation. I will, therefore, have a traditional wedding.” Bien Alisema.

Baadhi ya wasanii walioimba ama kuwatumbuiza wageni wa Chiki na Bien ni msanii Nameless,Sauti sol,Nazii na pia Nyashinski ambaye aliimba wimbo wake wa Mungu pekee, harusi hiyo ilikuwa ya kuvutia.

Hamna mtu yeyote ambaye aliruhusiwa kubeba simu katika sherehe hiyo kwa maana walitaka akili zao ziwe kwenye sherehe na si kuchukua picha na video kupia kwa simu zao.

Bien alimchumbia Chiki mwaka jana katika sherehe ya siri pia,katika mkahawa wa wastegate Nairobi, alilipia mkahawa huo wote ili aweze kumchumbia kipenzi cha roho yake.

Alihakikisha kuwa sherehe hiyo ilihudhuriwa na marafiki wake wachache.