Kwendeni huko! Nina haki ya kusikika, Murkomen afoka kwenye uzinduzi wa BBI

Murkomen
Murkomen
Kiongozi wa walio wengi katika Seneti Kipchumba Murkomen amekatisha kwa muda halfa ya uzinduzi wa ripoti ya BBI baada ya kulalamikia mpangilio wa jinsi shughuli hiyo inavyoendeshwa.

Alipotwaa jukwaani kuzungumza, Murkomen alilalamika kwamba ratiba ya halfa hiyo imefanywa kwa mapendeleo huku baadhi ya viongozi wakinyimwa fursa ya kuzungumza.

"Lazima tuseme ukweli, hata jinsi Junet anavyosimamia hafla hii haoneshi usawa. Hiki ni kipindi cha kusikiza maoni ya viongozi," Murkomen alisema.

Aidha aliongeza kuwa: "Ili kujenga taifa hili kwa uaminifu, lazima tuwape fursa viongozi wengine kusikika. Hakuna vile nitaambiwa kutulia. Nataka kusikizwa."

Mratibu wa vipindi katika halfa hiyo mbunge wa Suna Mashariki Junet Mohammed alijaribu kumtuliza lakini Seneta Kipchumba Murkomen hakukoma.

"Subiri, tulia. Nataka kusikizwa," Murkomen alisema.

Baadhi ya wajumbe walianza kumnyamaza lakini Murkomen alipasa sauti yake kwa nguvu zaidi.

"Ni nani aliyewaalika watu waje hapa jukwaani ? Nimelala saa 4 asubuhi baada ya kusoma ripoti ya BBI usiku kucha," Murkomen alisema.

Ilimbidi mwenyekiti wa jopo la BBI Yusuf Haji kuingilia kati na kusihi umati kumpa nafasi ajieleze.

"Mpeeni huyu time aseme yake," Yusuf Haji alisema.

Hata hivyo Murkomen aliwapongeza jopo liliounda ripoti ya BBI ambayo kulingana naye anasema kwamba imefafanuliwa ipassavyo.

"Mungu aibariki Kenya. Kwendeni huko," seneta alisema.