Kyle McCarter atoa tamko kuhusu mapendekezo ya BBI

Screenshot_from_2019_11_29_16_17_12__1575033462_61036
Screenshot_from_2019_11_29_16_17_12__1575033462_61036
Balozi wa marekani hapa nchini Kyle McCarter amesema kuwa kuna haja kubwa ya mapendezo ya BBI kujadiliwa na wananchi kabla uamuzi kufanyika.

"Wananchi wanatakiwa kuisoma, wajadiliane kuhusu mapendekezo na baadaye kutoa uamuzi wao..."

 McCarter alikuwa mgeni katika kituo hiki mapema leo asubuhi,

Balozi huyu alisisitiza kuwa mapendekezo ya BBI yanaweza yakafanya vizuri iwapo mjadala wa kutosheleza utafanyika,

"Kilichonifurahisha kuhusu BBI ni kuwa mapendekezo yanazungumzia watu na jinsi wanavyoweza kubadilika..." McCarter

Kuhusu taarifa za kumzuilia Amos Wako kutembelea Marekani, Kyle amesema kuwa Marekani ina ushahidi wa kutosha kufanya hivyo,

"Hatuwezi tukafikia uamuzi kama huo kama hatuna ushahidi..."

Aidha, kiongozi huyu amesema kuwa wanafuata sheria kufanya hivyo,

"Tunaweza tukawataja kwa mujibu wa sheria..." Kyle

Kyle aliteuliwa na rais Trump kuwa balozi wa Kenya January 2, 2019.

Kuhusu vita dhidi ya ugaidi, Kyle amesema kuwa Marekani inasaidiana na Kenya kukomesha wanamgambo wa Alshabaab,

"Tunafanya kazi na Kenya ili kuhakikisha tunazima wanamgambo wa Alshabaab pamoja na kuipa nguvu jeshi..."

Kuhusu ufahamu wa lugha ya Kiswahili na vyakula nchini, Kyle amesema kuwa anapenda sana ugali,

"Nakula ugali, najua kidogo lakini najaribu... nitajitahidi sana kuelewa kiswahili."  Kyle alisema.

Kyle amezungumzia nafasi chache za kazi nchini na kuhimiza vijana wapewe nafasi za ajira,

"Naamini na nikona maono makubwa sana kwa Kenya. Kenya ina uwezo na kuna vijana wengi ambao wamesoma na wana tajriba ya kazi kwa hivyo tunatakiwa tuwape nafasi."