Lala salama: Daktari mkenya aaga dunia kutokana na virusi vya corona

Familia, marafiki na hata madaktari kwa jumla wamekumbwa na majonzi baada ya kumpoteza Daktari Doreen Adisa Lugaliki kutokana na maradhi ya virusi vya corona

Adisa alikata roho Ijumaa Julai 10 majira ya asubuhi na ameombolezwa na madaktari wenzake kwenye mitandao ya kijamii kuwa mtu mkarimu. Kulingana na daktari Mercy Korir, Adisa alikuwa mwenye hekima na angewajibikia kazi yake bila kusukumwa wala kusimamiwa.

" Tumempoteza daktari aliyeonyesha bidii katika utendakazi wake kutokana na virusi vya COVID-19, Mola ailaze roho yake mahala pema." Alizungumza Korir.

Kutoka kwetu wanajambo Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.