Loss:Kampuni za  Michezo  ya kubashiri zapoteza  kesi dhidi ya KRA .

Mahakama kuu  huko Nanyuki  imefafanua  kuhusu tafisiri kamili ya jina ‘Pesa anazoshinda mtu’ katika michezo ya kubashiri  kama inavyotumiwa na KRA  wakati wa kuamua  kodi inayolipwa na kampuni za michezo ya bahati nasibu . KRA  hutoza kodi ya asilimia 20  ya kiasi kinachotolewa kwa mchezo huo na asilimia 20 ya kiasi kinachopatikana baada ya ushindi .

Maana ya jina hilo iliwasilishwa kortini mwaka wa 2018 na mtu moja wa kushiriki michezo ya kubashiri  Lesaloi Selelo,  ambaye alidai kwamba kutoza kodi kwa kiasi cha fedha alizoshinda mtu anayeshiriki mchezo huo ni ukiukaji wa katiba .Pevans E. A. Limited, Bluejay Limited na Acumen Communication Limited  ambao walihusishwa katika kesi hiyo  walidai kwamba pesa anazoshinda mtu katika michezo hiyo sio mapato na hazifai kutozwa kodi .Betway baadaye iliwasilisha kesi kama hiyo mwaka wa 2018  ili kupata tafisiri ya  ‘pesa anazoshinda mtu ‘ lakini kesi hizo zikajumuishwa kuwa moja kwa sababu zilikuwa zikishughulikia  masuala yanayofanana .

Mahakama ilifutilia mbali kesi hiyo siku ya  alhamisi  hatua inayomaanisha kwamba tafisiri ya KRA kuhusu pesa alizoshinda mtu katika michezo ya kubashiri zitatozwa kodi .KRA  ilizidhiinisha kampuni 10 mbazo hazikupewa upya leseni Julai tarehe moja  kwa sababu ya maswali kuhusu utekelezwaji wa kanuni za ulipaji kodi.Betway, OdiBets, Mozzartbet, Ken Bookmakers, Lucky 2u, Eazi Bet, Kick off, Eastleighbet, Palms Bet na  Bet  zilipokea idhini ya kuhudumu Julai tarehe 22 lakini   Betin na SportPesa,  ambazo ni miongoni mwa kampuni kubwa za michezo ya kubashiri  hazikuwa katika orodha ya KRA ya kampuni zenye idhini ya kuhudumu .