Maadhimisho ya miaka 10 ya Diamond Platnumz kwenye muziki, mchango wake

Screenshot_from_2019_12_29_14_21_39__1577618521_89635
Screenshot_from_2019_12_29_14_21_39__1577618521_89635
Msanii wa kizazi kipya na mkurugenzi wa lebo ya WCB Diamond Platnumz anatazamiwa kufanya bonge la tamasha mjini Kigoma ili kuadhimisha miaka 10 ya uchapakazi katika tasnia ya muziki.

Sherehe hii itafanyika kwao Kigoma na ameweza kuwaalika wengi ili kuwapa burudani tele.

https://www.instagram.com/p/B6lr6JyJciQ/

Kama kawaida safari yoyote huwa imejaa milima na mabonde na wakati mwingine wengi hukatishwa tamaa.

Diamond ameweza kuipamba sherehe hii na kuita mastaa wengi Tanzania.

Aidha, staa huyu ameanzisha hashtegi kwa jina #Twezetu Kigoma ili kuwavuta wengi ukumbi wa Kigoma.

Safari ya muziki ya nyota huyu wa bongo fleva ilianza mwaka wa 2009 na kufikia sasa amepiga hatua kubwa pamoja na kuupeleka muziki wa afrika mashariki katika upeo wa juu zaidi.

Diamond ameweza kutoa mchango mkubwa katika jamii huku akiwatoa kimuziki mastaa kama Harmonize, Rayvanny, Queen Darleen, Mbosso pamoja na Lavalava.

Kando na mchango huo wa kupigiwa mfano , Diamond ametengeneza ajira kwa wanahabari kwa kuanzisha kituo cha redio na runinga Wasafi FM na Wasafi TV mtawalia.