Maafisa wa DCI kuhoji wafanyakazi kutoka afisi ya William Ruto.

Hatimaye wafanyakazi wanne kutoka afisi ya  naibu rais William Ruto watahojiwa na maafisa wa ujasusi kutoka DCI kuhusiana na mauji ya  Kipyegon Kenei.

Makachero hao wanaofanya uchunguzi huo, watawachunguza watu wengine watano  ikiwemo wafanyakazi wawili wamawasiliano wanaoaminika walifuta data za simu ya Kenei.

Frank Kipyegon Kenei,alipatikana ameaga nyumbani kwake februari,20, huku mauaji yake yakiibua maswali ambayo hadi leo hayajajibiwa.

Kenei alizikwa jumamosi iliopita nyumbani kwake kaunti ya Nakuru na  aliacha mjane mmoja na watoto wawili

Wapelelzi hao walisema kuwa washaapata watu tisa  ambao watachunguzwa kuhusiana na kesi hiyo, mmoja wa wakuu wa  wapelelezi alipoulizwa kama wamempata aliye muua Kenei alisema'be patient'

Ripoti zinasema kuwa wauaji hao wlionekana barabara kuu ya Mombasa Kenei akiwa amezirai na kisha kumpiga risasi na kumrudisha kwa nyumba yake.