Maafisa wa usalama vitengo tofauti ni miongoni mwa watu waliowekwa kwenye karanti ya lazima-Hussein Dhadho asema

EW1pNMmXkAApKtx
EW1pNMmXkAApKtx
NA NICKSON TOSI

Katibu msimamizi katika wizara ya usalama wa ndani Hussein Dhadho amesema maafisa wa usalama kutoka vitengo tofauti takriban 52,ni miongoni mwa watu 1254 waliowekwa kwenye karantini ya lazima hiyo jana baada ya kukiuka amri ya serikali ya kuwa kwa nyumba kufikia mida ya saa 7 jioni.

Yakiji hayo aliyekuwa meneja mtendaji wa shirika la kutathmini ubora wa nyama nchini Kenya Meat Commission Ibrahim Haji ametakiwa kulipa milioni 11.5 kwa shiriko hilo.

Mahakama kuu imetoa uamuzi huo hii leo baada ya Haji kupatikana na makosa ya matumizi mabaya ya ofisi.

Kwengineko ni kwamba chuo kikuu cha Dedan Kimathi kitalazimika kuanda hafla ya kufuzu kwa mahafala kupitia kwenye mitandao ya kijamii kama Facebook na Youtube.

Mkusanyiko tu wa habari ambazo zimegongwa vichwa vya habari mida hii.