Wakili wao Danstan Omari siku jumatano amesema pia watamtaka kiongozi wa ODM Raila Odinga kutoa taarifa . Raila na Uhuru walinaswa katika picha hiyo ya Video wakizuru miradi mbali mbali inayoetekelezwa CBD .
Omari amesema wateja wake watazitumia taarifa hizo kama utetezi kwani wamepoteza kazi zao kwa ajili ya kesi hiyo .
Patrick Rading na Janet Magoma walifikishwa kortini jumatano na kushtakiwa kwa kukiuka sharia za kutumia vibaya komputa na uhalifu wa mtandaoni .
Omari amemuambia hakimu Bernad Ochoi kwamba wateja wake hawakukiuka sharia yoyote kwani walikuwa tu wanaonyesha ‘uzalendo’
Inadaiwa wawili hao mwendo wa saa mbili na dakika 20 juni tarehe 2 waliichukua picha hiyo ya video iliyowaonyesha rais Kenyatta na msafara wae katika barabara ya Kenyatta .
Serikali haikupinga kuachiliwa kwao kwa dhamana na kuutaka upande wa utetezi kutoa ushahidi wa kuonyesha kwamba wateja wao wamepoteza kazi zao .
Waliachiliwa kwa dhamana ya shilingi elfu kumi pesa taslimu