Maajabu! Bobi Wine ashtakiwa kwa kupanga kumkasirisha Museveni

BOBI WINE
BOBI WINE
Mbunge ambaye pia ni mwanamzviki nchini Uganda Bobi Wine ameshtakiwa kwa kupanga njama za kumkasirisha au kumkejeli rais Yoweri Museveni.

Hili shtaka jipya limeongeza kwa lile la awali la uhaini. Katika tukio hilo lililopelekea kuakamatwa kwake, yeye na wenzake wanashtumiwa kwa kurushia mawe msafara wa rais Museveni mwaka 2018 wakati wa mkutano wa kampeni katika mji wa Arua ulioko kaskazini mwa Uganda.

Wine anakabiliwa na kifungo cha hadi maisha ikiwa atapatikana na hatia. Wine na wenzake wengi wanadai kuteswa wakiwa korokoroni, madai ambayo mamlaka nchini humo imepinga.

Bobi Wine ambaye jina lake halisi ni Robert Kyagulanyi, bado anakabiliwa na mashtaka katika mahakama nyingine, kwa kufanya maandamano kupinga ushuru uliowekewa matumizi ya simu kwa shughuli za kifedha na matumizi ya mitandao ya kijamii mwaka 2018.

Mwandishi Mochama kulipwa fidia ya milioni 9, kwa kuharibiwa jina

Bobi amejitokeza kama mpinzani mkuu wa utawala wa miongo mitatu wa rais Yoweri Museveni. Hivi majuzi alitangaza kuania urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2021.