Maambukizi ya corona yafika 10,105 huku wakenya wengi wakianza kupuuza maagizo ya kuzuia ugonjwa huo

Licha ya hatari  inayozidi  kuongezeka ya  maambukizi ya virusi vya corona, wakenya  wengi wanazidi kupuuza masharti  yote wanayofaa kuzingatia ili kuzuia maambukizi  zaidi. Maelfu wanazidi kwenda mashambani huku wengi wakisusia kuvalia maski.

Tathmini yaonyesha pia kwamba wengi wamepuuza uhitaji wa kuosha mikono kama njia moja ya kukabiliana na virusi vya corona. Skiza Podi hii inayoeleza baadhi ya vitu ambavyo  wakenya wanafanya vinavyohatarisha uwezo wao kupata ugonjwa wa corona.

&t=251s

Tangu serikali  ilipotangaza kufungua kaunti ya Nairobi na kuruhusu usafiri wa kuingia na kutoka jijini, yamkini watu wengi wamelichukulia jambo hilo  kumaanisha kwamba  tumefaulu kukabiliana na virsi vya corona.  Imeibuka pia kwamba baadhi ya wakenya sasa wameanza kupuuza hatari ya ugonjwa huo licha ya kwamba hadi kufikia sasa, zaidi ya watu 185 wameaga dunia.

Kuna  hofu kwamba ongezeko la maambuziki zaidi ya ugonjwa huo huenda likaifanya serikali kurejesha hatua  kali za kuzuia usafiri wa watu kutoka kaunti moja hadi nyingine na hata kutangaza marufuku za kutotoka nje katika baadhi ya maeneo. Tangu kutolewa kwa ruhusua ya usafiri wa kutoka kaunti moja hadi nyingine visa vya ugonjwa huo havijapungua na rais Kenyatta akitoa tangazo hilo alisema endapo hali itazidi na kuwa mbaya hatosita kurejesha vikwazo vikali zaidi .

Kuna maeneo ama shughuli ambazo  zinakutia katika hatari ya kuambukizwa corona .Fahamu hapa kuhusu hatari unayojitia kwa kushiriki shughuli hizo ama kwenda katika  maeneo hayo

&t=36s