Takribani Wakenya 32 walikuwa wameabiri ndege ya Boeing 737-Max wakati wa janga la Machi 10, ambalo liliwauwa abiria wote157.
Familia za wahasiriwa wa ajali hiyo zilikuwa JKIA mapema asubuhi wakisubiri kukabidhiwa mabaki hayo ya jamaa zao.
Ripoti ya awali iliyotolewa mnamo Aprili ilionyesha kuwa marubani wa Ethiopia Airlines walipambana na mfumo wa kompyuta ambao uliamuru ncha ya mbele ya ndege kutazama chini kwa sababu ya data mbaya ya sensa.
Mfumo huo wa sensa ya Kopmyuta ulitajwa kusababisha ajali nyingine ya ndege katika Indonesia, ambayo iliwauwa watu 189.
Familia ya wahasiriwa ya Kenya ilikuwa imewasilisha mashtaka huko Chicago mnamo Aprili dhidi ya kampuni hiyo ya ndege ya Marekani, Boeing 737-max8 kwa ajali hiyo.
George Kabau alisema anataka kulazimisha kampuni hiyo kutoa hati na barua pepe zinazohusiana na mfumo wa ndege ya 737 MAX 8, ambayo ilitengenezwa ulimwenguni pote baada ya ndege kuu mbili kuanguka nchini Ethiopia na Indonesia.
Mnamo Julai, Kenya iliambia Bunge la Marekani kwamba Boeing ilikuwa bado haijaomba msamaha wa kibinafsi kwa familia za wale walioathiriwa.
Lakini kwa kuzingatia Mkataba wa Montreal, kila familia ya wahathiriwa wa ajali ya ndege hiyo inafaa kupokea kitia cha shilingi milioni 17.
Mkataba huo, uliopitishwa na Shirika la Kimataifa la ndege, unasema kwamba "ikiwa ndege itapatikana na kosa kwa kusababisha ajali, kila abiria aliyeathiriwa atapata thamani isiyopungua $ 113,100.