Madereva wa masafa marefu watishia kuandamana kutokana na dhulma za maafisa wa usalama Uganda

NA NICKSON TOSI

Mzozo wa kibiashara unatazamiwa kuibuka baina ya Kenya na Tanzania baada ya madai kuibuka kuwa madereva wa masafa marefu wanaotoka nchini Kenya wananyanyaswa na kubaguliwa na maafisa wa usalama kutoka nchi jirani ya Uganda.

Madereva hao sasa wamesema kuwa wanapania kuandama ili kushinikiza maafisa hao wa Uganda katika mpaka wa Busia na Malaba wanachukuliwa hatua kutokana na dhulma ambazo wanazipitia mikononi mwao.

Jana katibu mkuu wa muungano wa madereva wa masafa marefu nchini Nicholas Mbugua aliwataka madereva hao kukoma kupeleka mizigo Uganda kwa kile alikisema ni dhulma wanazopitia wakenya hao.

Mbugua amesema kuwa madereva hao wanapofika Uganda wananyimwa chakula, maji na mahali pa kulala.

“Our drivers are being harassed so what I am saying is, stop going into Uganda. Let them come for their own cargo,”alisema Mbugua

“Who said Ugandans cannot have the virus? We are going to stop going into Uganda until the two governments agree on how to address these issues,”ameongeza Mbugua.

Kwa sasa, kuna malori ya kubeba mizigo takriban 600-1,000 yanayosafirisha mizigo baina ya mataifa ya Uganda, Rwanda, Burundi, South Sudan na  DR Congo kutoka kwa bandari kuu ya Mombasa.