Madiwani wa zamani wadai fidia ya shilingi milioni 1.5 kila mmoja

Picha: savvykenya.com

Waliokuwa madiwani kabla ya mfumo wa ugatuzi kubuniwa wanaitaka serikali kuwapa kiinua mgongo cha shilingi milioni moja nukta tano kila mmoja.

Madiwani hao wakiongozwa na mwenyekiti John Orwenjo wanasema wao kama madiwani walichangia pakubwa katika kukuza uchumi wa nchi mashinani na itakuwa vyema wakipewa kiinua mgongo.

Aliongezea kuwa kwa sasa baadhi ya madiwani wanaishi katika hali ya uchochole na bila usaidizi wa serikali kuu au za kaunti na basi wataishia kusahaulika bila fidia.

Aidha swala la fidia limekuwa na utata hasa kwa wanasiasa, huku serikali ikidai kuwa wale wote wanao lenga kunufaika lazima wajiuzulu kabisa kutoka katika ulingo wa siasa.