Maeneo 10 Ya Kustaajabisha Yaliyo na Ulinzi Mkali Sana Duniani

Iwapo ushawajiuliza ni maeneo yapi yalio na ulinzi mkali sana ulimwenguni na kwa sababu gani basi hapa kuna orodha na maelezo ya swali hilo.

Kila kitu chochote cha thamani, chenye tishio la kuangamizwa  au kinachoadimika ulimwenguni kinahitaji kupewa ulinzi wa kila aina. Ifuatayo ni orodha ya maeneo hayo 10 pamoja na sababu za kupewa ulinzi mkali.

1. Area 51, Nevada Marekani

Hii ni sehemu ambayo ni  mafuruku kwa umma kukaribia.

Inaaminika kuwa na angatua ya kijeshi ya Edward ambayo imeangaziwa  sana kuwa yenye usiri mkubwa

Hii ni kwa kuwa yanayoendelea katika eneo hilo hayajawekwa hadharani.

Kutokana na usiri huu, umevutia watu wengi sana.

Ua wa makaazi hayo una sensa zinazonasa binadamu au kitu chochote kinachotembea au kukaribia eneo hilo.

Pia washika doria wenye silaha kali  huzunguka eneo hilo wakiwa imara kukabiliana na yeyote anayekaribia.

2. Ngome ya Knox, Marekani

Ngome  hii inahifadhi akiba na hazina ya Marekani na miongoni mwa maeneo yanayolindwa sana duniani.

Fort Knox inalindwa sana wakati wowote na walinzi wenye silaha hatari.

Hakuna yeyote anayeruhusiwa mahali pale isipokuwa una mwaliko rasmi.

3. Ikulu ya White House, Marekani

Makao haya ya marais wa Marekani inabakia kuwa mojawapo ya majengo yanayolindwa zaidi ulimwenguni. Uzio wa chuma huzunguka  jengo hilo ambalo limejengwa na ukuta mpana sana.

Madirisha ya majengo hayo ya rais haupenyezi risasi  huku maafisa wa hali ya juu wa kijasusi huzingira na kuilnda makazi hayo kwa hali na mali.

4.  Makavazi ya Kisiri ya Vatican, Italia

Kituo hiki ni cha kuhifadhi mali mali yenye thamani ya jadi, hati maalum ya kiserikali pamoja na leja muhimu kutoka kanisa la Kikatoliki.

Makavazi haya yalitengwa kutoka maktaba ya Vatican na umilizi wake na upokezi  huwa ni kutoka Papa Mtakatifu  mmoja hadi mwingine.

5. Federal Reserve Bank of New York

Hizi ni benki muhimu sana ulimwenguni.

Kuna benki 12 za Hifadhi ya Shirikisho zilizoko nchini Marekani.

Maeneo hayo yote hupewa ulinzi wa hali ya juu sana kutokana na kuwa sehemu muhimu ya kuhifadhi pato la taifa na uchumi wa taifa la Marekani.

Robotiki hutumika katika Hifadhi hii huku kikosi hatari ya jeshi wakilinda nje  na ndani ya jengo hilo.

6. Svalbard Global Seed Vault, Norway

La kustaajabisha ni kwamba eneo hili hulindwa kusudi alke likiwa ni kuhifadhi  sampuli  mbegu muhimu ya mimea na vyakula adimu.

Lengo la kulindwa kwa eneo hili ni kuhakisha kwamba vizazi vijavyo havitaangamizwa na baa la njaa.

7.  Mto Tumen 

Maeneo haya ya mto hutumika kama lango  kuu kati ya mataifa ya Uchina, Korea Kaskazini na Urusi.

Sababu ya kulindwa zaidi ni kuwazua wakimbizi au maharamia wanaongia China kupitia mto huu usio na maji mengi sana.

8. Granite Mountain Records Vault

Kanisa  la Yesu Kristo la Siku ya Agano Jipya linamiliki  rekodi na historia nyingi ya enzi za kale.

Jengo hili limejengwa futi kadhaa ndani ya Mlima wa Utah.

Mazingira na  hali ya hewa katika eneo hili hudhibitiwa na teknoljia hili kuzua hati na madaftari muhimu kuharibiwa na mabadiliko ya mazingira.

9.  Megesho ya MaGari ya Bold Lane

Magari huegeshewa katika eneo hili la Uingereza. Ila cha kustaajabisha ni kwamba hakuna yeyote anayeruhusiwa bila idhini, isitoshe wakati wa dharura uzio wa eneo hili pamoja na milango yake hujifunga.

Limelindwa na vyombo vya uslama kutokana na uhalifu na soko la dawa za kulevya uliokuwa umekithiri.

10. Cheyenne Mountain Complex, Marekani

Jumba hili lilio na ofisi nyingi za kiserikali linapewa ulinzi wa juu sana.

Hapo awali ilikuwa nyumba ya mradi wa ulinzi wa anga Marekani na Kanada.

Ukuta wa jengo hili una futi  2,000 ya madini ya granite dhabiti.