Wamesema sio haki kwa maseneta kuanza kumshambulia Oparanya kuhusu uamuzi wa kusitisha huduma katika kaunti zote kwa ajili ya ukosefu wa fedha ilhali hatua hiyo ilichukuliwa na baraza la magavana bali sio na oparanya pekee .
Wawili hao wamesema wafanyikazi wa kaunti wamekuwa wakifanya kazi kwa miezi mitatu bila malipo na ni vyema iwapo watapumzika hadi walipwe pesa zao .
Oparanya akitangaza uamuzi huo siku ya jumatano amesema hatua hiyo imechukuliwa kwa ajili ya ukosefu wa fedha baada ya maseneta kukoa kuafikiana kuhusu mfumo wa kutumiwa katika ugavi wa fedha kwa serikali za kaunti .
Alisema kwamba vituo vya afya vya kaunti havitawasajili wagonjwa wengine na vitatoa tu huduma adimu kwa wagonjwa wa kutibiwa na kurejea nyumbani huku wafanyikazi wa kaunti wakitakiwa kuchukua mapumziko ya wiki mbili .
Oparanya amesema njia pekee ya kusuluhisha tatizo hilo ni kwa hazina ya kitaifa kutoa fedha kwa serikali za kaunti haraka . Maseneta hata hivyo wameonakana kukerwa na uamuzi huo wa COG na kuanza kumshambulia Oparanya .
Baadhi ya maseneta wamemtaja kama msaliti huku wengine wakimuita mwongo kwa kuongoza walicotaja kama kundi la ‘vijana’ wanaoshambulia bunge la senateambalo limekuwa likitetea kabisa ugatuzi .
Wamesema COG chini ya uongozi wa oparanya imegeuzwa kuwa sehemu ya serikali kuu na kuisaliti senate ambayo imekuwa ikipagania mgao wa fedha Zaidi kwa serikali za kaunti .